Mwenyekiti wa Umoja wa Madhehebu ya Kikristo (CCT) Mkoa wa Kigoma Askofu Dkt. Sospeter Ndenza kwa niaba ya Umoja huo amesema kwa kauli moja wanalaani vitendo vya uwepo wa shughuli za wapiga ramli chonganishi maarufu Kamchape mkoni hapa kwani zinachangia kwa kiasi kikubwa kuvuruga Amani na utulivu kwa wakazi.
Tamko hilo limetolewa na kiongozi huyo wa jumuia hiyo leo Februari 5, 2024, mara baada ikiwa ni Tamko Rasmi la Umoja huo likilenga kuhamasisha waumini wa madhehebu wanayoyaongoza kutokwenda kinyume Imani zao za kidini kwa kujihusisha na Imani za kishirikina ikiwemo upigaji ramli.
‘’Tumekutana hapa na kujadili kwa kina suala hili la waumini wenu kujikita katika kuamini watu wanaoitwa Kamchape, jambo hili halikubaliki na kwa kauli moja tunalaani vitendo hivyo na tunawaonya waumini wa madhehebu ya kikristo kutojihusisha na vitendo hivyo’’ Amesema.
‘’Sisi madhehebu ya kikristo Kwa kauli moja hatukubaliani, hatuungi mkono na tumakemea kwa nguvu na tunaungana na serikali katika kupiga vita vitendo hivyo kuendelea kufanyika katika Jamii, na tunawakaribisha Polisi Jamii kupitia madhabahu za makanisa yetu ili wawasaidie wakristo kuelewa kuwa kushirikiana na wapiga ramli chonganishi ni kinyume na sharia za nchi’’ amesisitiza Askofu Sospeter Ndenza.
Aidha Askofu Ndenza amepiga marufuku waumini wa madhehebu yaliyo chini ya jumuia hiyo kushiriki katika shughuli zote zinazohusiana na Kamchape huku akisisitiza marufuku hiyo kwa wapiga ramli hao kusogelea nyumba za Ibada pamoja na viongozi wa dini.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amesema Serikali itanendelea kuchukua hatua kali dhidi ya watu wote watakaobainika kuvunja sharia kwa kujihusisha na Kamchape katika kuvunja Amani na kuharibu mali za watu wengine ili kutekeleza makusudio ya kundi hilo.
Aidha ameitaka jamii kuchukua tahadhari dhidi ya watu hao kwani ni matapeli na wanachokifanya ni kuulaghai Umma kisha kuwachukulia wanajamii fedha zao.
PICHA YA PAMOJA YA MKUU WA MKOA WA KIGOMA (WA TATU KUTOKA KULIA) AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA UONGOZI WA CCT KIGOMA, MARA BAADA BAADA YA KIKAO KILICHOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA OFISI YA MKUU WA MKOA WA KIGOMA FEB 5,2024.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255738192977
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa